Mbunge
wa Iringa mjini kupitia tiketi ya Chadema, Mch. Peter Msigwa amezidi kukana
madai ya kumtelekeza mtoto na kueleza kuwa taarifa hizo zinaenezwa na Jerry
Muro.
Akizungumza
na EATV, Mch. Msigwa amesema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na kueleza
iwapo lisemwalo lipo basi muhusika amtafute katika namba aliyoitoa na
ikishindikana amfuate Bungeni.
“Mimi
nitamtambuaje huyo mtoto, hiyo picha wameweka tu, ilipoanzia ni kwa Jerry Muro
ndio ameanza kusambaza hizo habari kwamba mimi ni mwanamke aliyeenda kwa
Makonda amejieleza ndio nimemuacha,” amesema Mch. Msigwa.
“Ninachokijibu
pale, nakijibu kitu ambacho ameanzisha Jerry Muro, kwamba kuna mtu nimemtelekeza
amekuwa akinitafauta na nimekuwa nikimzuia, nimejibu kwamba kama huyo mtu huyo
yupo nimekuwa nikitoa namba zangu za simu na kama sipatikani aje hapa Bungeni,”
amesisitiza.
Kuanzia
mwanzo mwa wiki hii mamia ya wanawake walijitokeza ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda ili kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na
wazazi wenzio. Pia RC Makonda ametoa nafasi ya kuwasikiliza wanaume
waliotelekezwa na wake zao ambapo watapatiwa msaada wa kisheria.
No comments:
Post a Comment