Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Marketing Executive

Sunday, June 3, 2018

SERIKALI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA HASA UHIFADHI WA MITI NA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA.


Katika kufanikisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira serikali ya Jamhuri ya Tanzania imefanikisha kuwepo kwa maonyesho ya matumizi ya nishati mbadala katika suala zima la matumizi ya mkaa unaotokana na taka,masalia ya viumbe hai(makaa ya mawe),na mabaki ya mbao.

Katika kufanikisha hilo Wizara ya Mazingira Nyumba na Makazi chini ya Mh January Makamba imetoa fursa kwa Taasisi,Asasi,za kiserikali na zisizo za serikali(binafsi) kuonyesha uwezo wa kuhakikisha miti inabaki salama kwa kuzalisha mkaa mbadala.

Maonyesho haya yanafanyika katika viwanja vya maonyesho MNAZI MMOJA jijini Dar  Es Salaam kwa muda wa siku 5.Maonyesho haya yamefunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kasim Majaliwa.

Katika maonyesho haya kuna mabanda zaidi ya 20 yanayotoa elimu ya matumizi ya nishati mbadala na utunzaji wa mazingira,kuendana na kauli mbiu ya mwaka NITUNZE NIKUTUNZE.

Baadhi ya wadau wanaoshiriki katika maonyesho haya ni AG ENERGIES, GREEN POWER GROUP,KIPEPEO RECYCLERS,ENVOTEC SERVICE LTD,ZAID RECYCLERS,BSM,MENA WOOD BRIQUETING CO.LTD,LISTAF ENTERPRISE SOLITION,MABAKI MALI,MKAA POA HALISI,MCHAU WINDMILL ENTERPRISES,DEMACO MOROGORO,WASTEWATER SOLUTIONS,EDO SAMA,TANZANIA BIOMIC CO.LTD,ALPECH,SIMUSOLAR,SIX STAR HOLDING LTD,ZOLA,OFISI YA MKUU WA MKOA WA SONGWE,TATC,TANPACK TISSUES LTD,GOODFIRE BRIQETTES,JIKO MATAWI,JHS,SUNKING,SIGA ENTERPRISES,FAMILY HERBAL CLINIC,TANZANIA AIRPORT AUTHORITY(TAA),WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MKAA ENDELEVU,MKAA MKOMBOZI,SNV,BORDA, na IDARA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA.

guta86.blogspot.com imefanikwa kutembelea maonyesho haya na kufanya mzungumzo na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa wadau hao.Edwin86 aliongea na Mr James,Jesca Elias na Gemma Kavishe wa Six Star Holding Ltd,Irene Missanga Muja(CEO) wa Mabaki Mali,Leah Nyengo wa Mena Wood Briqueting Co.Ltd,Mr Godlove Ngoda wa BORDA,na wengine wengi.Pia Edwin86 amekutana na  kufanya mazungumzo na Mh John Hagu Mratibu Mkuu wa UWAMITA (Mifuko mbadala Tanzania)
Kilele cha maonyesho haya ni tarehe 5//2018 hapa hapa Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.
Imeandaliwa na Kulipotiwa na Edwin86 wa guta86.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment