JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS
TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI
YA MKUU WA MKOA WA SONGWE
1:0 UTANGULIZI
Mkoa wa Songwe upo eneo la Nyanda za Juu Kusini
Magharibi mwa Tanzania. Mkoa una kilometa za mraba 27,656 sawa na asilimia 3.1
ya eneo lote la Tanzania ukiwa na latitudo 7º na 9º 36’ kusini ya Ikweta na longitudo kati ya 32º na 33º 41’ Mashariki ya
Greenwich. Mkoa unapakana na nchi za
Zambia na Malawi upande wa Kusini, Mikoa wa Rukwa na Katavi upande wa Magharibi, Kaskazini na Mashariki
Mkoa wa Tabora na Mbeya.
Mkoa una Wilaya 4,
Halmashauri 5, Tarafa 12, Kata 94, Vijiji 307, vitongoji 1,493, Mitaa 71, jumla ya kaya 226,428 na jumla ya
watu 1,125,520.
2. MAKAA YA MAWE
Makaa ya mawe ni aina
ya mwamba mashapo au mwamba metamofia na fueli kisukuu muhimu. Mwamba ulitokea kutokana na mabaki ya mimea ya kale yaliyogeuzwa kuwa
aina ya mwamba katika mchakato wa miaka mamilioni. Kikemia makaa ya mawe ni kaboni.
Asili ya makaa ya mawe ni mabaki ya mimea iliyokufa miaka mingi iliyopita.
Mabaki ya mimea yanapofunikwa kwa maji au kuzama katika matope hayaozi kama jinsi ilivyo kutokea kwa mboji. Kinachotokea ni ganda la nyuzi za
mimea zinazokauka wakati maji yanapopungua. Maganda haya ni kitangulizi cha
makaa ya mawe. Ubora wa kiuchumi na kiwango cha nishati kilichomo katika makaa
unaongezeka kadri ya umri wake na kina cha mahali panapochimbwa
Mkoa wa Songwe una makaa wa
mawe katika wilaya ya Mbozi, Ileje na Songwe ambayo ni Magamba, Kiwira na
Kabul.
3. UTENGENEZAJI
WA MKAA
Teknolojia ya utengenezaji wa mkaa bora wa kupikia ni
teknolojia inayopatikana wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe katika machimbo ya Makaa
ya Mawe ya Magamba. Utafiti ulifanyika
mwaka 2017 na Mchumi Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Kitengo cha ubora wa Makaa ya mawe kutoka
Tancoal Energy Limited kilichopo mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
Matokeo ya teknolojia hii yanatoa
jibu la matatizo yaliyodumu kwa muda mrefu yaliyotokana na ukataji miti
kiholela kwa ajili ya matumizi ya nishati.Teknolojia ya Makaa bora ya briketi ni rahisi, na ni mbadala wa nishati,
ni suluhisho kwa kero za kuni na mkaa kwa matatizo
mateso yatokanayo na
nishati hizo zitumikazo kwa matumizi ya nyumbani na katika taasisi mbalimbali.
Mkaa unatengenezwa kwa mchanganyiko wa
chenga chenga ( vumbi) la makaa ya mawe , udongo mfinyanzi, virutubisho, mabaki ya mazao ya
kilimo yaliyokauka na maji katika vipimo maalumu.
Briketi za makaa ya mawe
zaweza kutengenezwa kwa mikono kwa kutumia kifaa kilichotengenezwa maalum kwa
bati gumu (hand molder).
3.2 MUDA WA KUKAUKA
Briketi za makaa bora huchukua muda wa
siku 2 au 3 kukauka kulingana na hali ya hewa baada ya kutengenezwa.
3.3
KIPINDI CHA MASIKA/ MVUA
Kipindi cha masika ni
rahisi njia mbadala ya kukausha nishati hii huweza kukaushwa katika tanuru, au
kivulini baada ya kutengenezwa.
No comments:
Post a Comment