Video
queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki Dunia
leo katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyoko Mwenge, Wilaya ya Kinondoni, jijini
Dar es Salaam.
Alikuwa
anasumbuliwa na Homa ya matumbo pamoja na tatizo la kupungukiwa na damu.
Akithibitisha
taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema
Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na
alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.
Tayari
mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji
Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Mungu
ailaze roho yake mahala pema peponi.
No comments:
Post a Comment