Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Marketing Executive

Sunday, June 3, 2018

BAKORA PIONEER YASAKA WADAU


Kundi mahiri la vichekesho lenye maskani yake Jijini Dar Es Salaam maeneo ya Tabata Chang’ombe linaendelea kufanya jitihada za dhati ili kuhakisha linafanikiwa kupata mdau ama wadau watakao lisapoti kundi hilo katika shughuli yake ya kuelimisha jamii.

BAKORA PIONEER wameweka wazi juu ya hilo kupitia kwa Marketing manager wao Mr Edwin Malima ambaye ameweza kuhudhulia maonyesho ya utunzaji wa mazingira yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Mr Edwin Malima amepata nafasi ya kukutana na baadhi ya CEO’S wa kampuni,taasisi na asasi mbalimbali za serikali na binafsi na kupewa nafasi ya kuzungumzia juu ya uhitaji wa kundi hilo.
BAKORA PIONEER wanahitaji mdhamini mwenye nia,lengo,utashi,uwezo,na haja ya kuendeleza vipaji kwa vijana akitambua kua ni ajira tosha.

Baadhi ya wadau wameonyesha mwitikio juu ya suala hilo na kuomb kuonana na Mr Edwin Malima ambae pia ni founder na CEO wa guta86.blogspot.com.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Mr Edwin Malima
simu na :- 0719 797 295 / 0686  971 676 au E-mail :86guta@gmail.com

No comments:

Post a Comment