Rai hiyo imetolewa baada ya mradi huu kufika katika hatua nzuri na stahiki kuruhusu wawekezaji wa ndani na nje kuanza kuwekeza ili kupanua wigo wa mradi huu lengo ikiwa ni kuongeza ajira,kukuza uchumi na kuhifadhi mazigira.
Wawekezaji ama wadau wa sekta ya biashara na viwanda wanakaribishwa kuja kuwekeza katika mradi wenye faida kubwa kiuchumi.Mradi huu wa uzalishaji wa mkaa wa majumbani maarufu kwa jina la Mkaa Songwe unaotokana na makaa ya mawe ni jibu tosha la utunzaji wa mazingira hasa katika ukataji miti.Pia huendana na kipato cha Watanzania walio wengi kwani hupatikana kwa gharama nafuu sana.
Wadau ama wawekezaji wanaweza kuwekeza katika suala zima la vifungashi(packaging),Matangazo,Uingizaji wa Mkaa Songwe nchi nzima sokoni(Marketing) na uwekezaji katika eneo zima la uongezaji wa mashine za kisasa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wateja.
kwa mawasiliano piga smu namba +255 719 797 295 or email address 86guta@gmail.com.
kwa mawasiliano piga smu namba +255 719 797 295 or email address 86guta@gmail.com.
No comments:
Post a Comment