Meneja wa club ya Man City Pep Guadiola amewaomba wachezaji wake kua makini na tulivu watakapokutana na club ya Liverpool wiki hii katika michuano ya UEFA Champions league.
Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Etihad stadium ili kupindua kichapo cha mabao 3-0 walichokipata dhidi ya majogoo hao.
Meneja huyo amesema hivyo akiwa anahojiwa na waandishi wa habari jijini Manchester baada ya kupata kichapo kingine mfululizo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Manchester United. Mechi hiyo iliisha kwa kichapo cha magoli 3-2.
No comments:
Post a Comment