Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Marketing Executive

Tuesday, April 17, 2018

SOUTHAMPTON WAMNYATIA WESTWOOD

Timu ya Southampton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ipo mbioni kuinasa sahihi ya mlinda mlango wa timu ya Sheffield Wednesday Kieren Westwood.

Wakali hao The Saints wameamua kufanya hivyo baada ya mlinda mlango wao Fraser Foster kubakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake wakuichezea timu hiyo.

Westwood mwenye umri wa miaka 33 atakuwa amecheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Leeds United. Pia timu ya Celtic imeonyesha nia yakuinasa sahihi ya mchezaji huyo.

Westwood amekua nje kwa miezi minne akisumbuliwa na maumivu ya paja na aliporejea mazoezini akakumbana na kuchanika kwa misuri ambako kumemweka nje hadi sasa, hali hiyo itamlazimu kukosa mechi zakirafiki dhidi ya Ufaransa, United States na Celtic.

No comments:

Post a Comment