Baadhi
ya maeneo ndani ya jiji la Dar Es Salaam yamekua na mlundikano wa taka na
kuvuruga shughuli zinazoendelea katika maeneo hayo.
Taka
hizo zinazotokana na uwepo wa
miundombinu mibovu ya uhifadhi wake zimekua kero kubwa kwa wakazi
husika.
Maeneo
yanayoathirika zaidi ni ya mabondeni kwani imekua ngumu kwa wahusika wa
ukusanyaji wa taka hizo kufika katika maeneo hayo.Suala zima linasababishwa na
upuuzwaji wa wahusika kuzingatia maeneo hayo kwa muda mrefu.
Wahusika
wamekua katika hali hizo kwa kutoa na kuelekeza nguvu zao maeneo ya pembezoni
mwa barabara tu kutokana na kutambua watu wengi huona taka za maeneo hayo na
kusahau maeneo ya ndani na mabondeni.
No comments:
Post a Comment