Makaa ya
mawe ni aina ya mwamba mashapo au mwamba metamofia na fueli kisukuu muhimu kwa
lugha ya kitaalamu kwa Kiswahili.
Ubora wa
kiuchumi na kiwango cha nishati kilichomo katika makaa unaongezeka kadri ya
umri wake na kina cha mahali panapo
chimbwa.
Mkoa wa
Songwe umekua maarufu kwa utoaji wa makaa ya mawe hasa katika wilaya ya
Mbozi,Ileje na Songwe ambayo ni Magamba,Kiwira na Kabul .
Bi Halima Mpita akiwa katika uzalishaji TIRDO jijini Dar es Salaam
Utengenezaji wa mkaa kwa matumizi bora ya kupikia
majumbani maarufu kama mkaa songwe ni teknolojia inayopatikana wilaya ya Mbozi
mkoani songwe katika machimbo ya makaa ya mawe ya MAGAMBA,na utafiti ulifanyika
mwaka 2017chini ya mtaalamu wetu na Mchumi mkuu wa Mkoa wa songwe Bi Halima
Mpita kwa kushirikiana na kitengo cha ubora wa makaa ya mawe kutoka Tancoal
Energy Limited kilichopo wilaya ya Mbinga mgodi wa Ngaka.
Bi Halima Mpita akiwa katika mgodi wa Ngaka
Teknolojia hii ni suluhisho kwa kero za kuni na
mkaa inayopelekea ukataji wa miti na kuharibu mazingira kwa ujumla jambo
linalochangia kuongeza hali ya ujangwa nchini,mvua zinazoambatana na
madhara,mabadiliko ya hali ya hewa,uharibifu wa makazi ya viumbe hai wa
porini,kuharibu vyanzo vya maji,na kuondoa uoto wa asili ,nk.
Mkaa Songwe unaotokana na makaa ya mawe
umetengenezwa kwa mchanganyiko wa chenga chenga[vumbi]la makaa ya mawe ,udongo
mfinyanzi,virutubisho,mabaki ya mazao ya kilimo yaliyokauka,na kuchanganywa na
maji katika kiwango maalumu.
KIPINDI
CHA MVUA
Mkaa songwe umekua suluhisho kwa wakazi wa mkoa
wa songwe kwani ni rahisi kukausha nishati hii kwa kutumia tanuru au kivulini
baada ya kutengenezwa na kutumika kwa kupikia.
UWAKAJI
Mkaa songwe mkaa bora wa mgodi wa Magamba huwaka
vizuri ,moto unapoanza kuwaka hutoa ulimi mfupi rangi ya bluu kutoka katika
jiko la kawaida ,mkaa songwe ukishawaka hautoi moshi wala kutengeneza masizi
ambayo yanachafua sufuria na vipande vidogo 34 vya mkaa huifadhi moto kwa saa 3
hadi 4 bila kuzima.
Mkaa songwe ni mkaa bora na safi kwa matumizi ya
kupikia unaowashwa kwaurahisi sana kama mkaa wa kawaida.
No comments:
Post a Comment